Thursday, 6 April 2017

KWA VIJANA WA KIUME MUNAOTAKA KUOA



Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo.
Japo kila mtu anakasoro zake ila kuna tabia ndogo ndogo ambazo huleta maharibiko kwenye mahusiano na kuufanya uhusiano kubadilika kutoka kwenye amani na utamu unaopaswa kuwa nao na kuwa mchungu iwapo mwanaume asipokuwa makini wakati wa uchaguzi wa mwenzi anaetaka kuwa naye na nimejaribu kufanya utafiti na kuongea na wanaume walioachana na wenzi wao pamoja na wale waliopigwa chini japo wanang'ang'ania wao ndo waliowatema wapenzi wao na kuongea nao kwa mapana juu ya nini kiliwafanya wafikia uwamuzi huo mzito wa kuachana na wenzi wao, ndipo tukapata maelezo mengi na kukuandalia wewe mpenzi msomaji wa kiumeni.com aina ya wanawake kumi ambao inakubidi kufikilia mara mbili kwa marefu na mapana kabla ya uwamuzi wa kuamua kumpa sehemu ya maisha yako.
1. Mwanamke Mchungu: Unamjua yule mwanamke ambaye huwa na hasira na jinsia ya kiume muda wote? Huwa haishi kulalamika wanaume huwa ni wapumbavu, mwanaume haaminiki ni kama mbwa, yeye hasira yake huwa ipo juu ya wanaume muda wote na anaona mwanaume hawafai na hawana umuhimu wowote, hii inawezeka inatokea labda sababu ya katendwa na kuvunjwa moyo mara nyingi, mwanamke wa aina hii iwapo akiwekwa ndani huwa ni vurugu, kukosea inatokea ila kwake itakuwa ni matusi na kosa moja dogo atalichukulia kwa uzito wa ajabu ambao hata haupo, akiwa na hasira ni kutukana na kutoa maneno ya chuki na kashifa kutokana na kutendwa kwake nyuma na wanaume na mrundikano wa hisia ambazo hajazitatua moyoni mwake na hasira zake huwa ni za karibu maana anakuwa hamuamini mwanaume wake hivyo yupo tayari tayari kuangalia kosa ili apate sababu.
2. Mwanamke Mchoyo: Ukiwa unahitaji nyumba iwe na furaha na mwenza ambaye anahitaji furaha yako na ya kwake pia, unahitajika sana kukaa mbali na mwanamke mchoyo, mwanamke wa namna hii yeye huwa anakuwa anajiweka mbele tu kuangalia masilahi yake bila kuangalia hisia zako na tofauti na hapo hata ndugu zako wakija sababu ya ile choyo anasababisha mvurugano wa familia na siku zote huwezi kujikuta na furaha zaidi ya kuwaza kutatua tatizo hili kabla hujalimaliza limeingia jingine.
3. Mwanamke Mpenda vitu: mwanamke huyu la kwake pesa, hajakiona hiki anakitaka, kile nacho anataka bila kuangalia hali ya kiuchumi imekaaje, kamuona jirani Mama Naniii kavaa vile na yeye anataka ashindane nae, anakuwa anajari zaidi vitu vya kidunia bila kuangalia familia yake ipo katika hali gani, yupo radhi kuvunja familia, kuvunja uaminifu wake kwako na hata ule wa kidini ili tu hali ya kile anachokuwa anakihitaji moyoni kitimie. Na siku zote huwa hawezi kuwa mwenza mzuri zaidi ya kukuumiza kichwa na kupasua nyongo yako kwa mawazo ya kumridhisha pale ambapo hauna uwezo napo.
4. Mwanamke Mtongozwaji: Umevutika na yule mwanamke ambae yeye huwa na ukaribu na wanaume mmoja au mwingine kupitiliza? Anacheka cheka na mwanaume huyu na yule kama lile limjusi la kwenye mawe linahama kutoka jiwe moja kwenda jingine likitikisa kichwa kwa kujikubali bila kujishitukia na kufanya wanaume wengi wajihisi labda wanapendwa na msichana wako. Inakubidi uwe mwangalifu maana mwanamke wa hivi huwezi kumfanya mwenza wako maana iwapo hata ukimuoa tabia za namna hii huwa ni ngumu kuziondoa na atakuhisi labda unawivu unamfatilia sana sababu ameisha kaa sana nje ya msitari mpaka hajui mwisho wa mipaka ni wapi. Ukimuoa mwanamke huyu usije shangaa kusikia mkeo anasifa ya kujichekelesha kwa wanaume wa mtaa wako.
5. Mama Shughuli: Huyu ni shida, kila aina ya sherehe yeye kaalikwa na zote anaziudhuria, Diamond anaimba kwenye klabu ya karibu saa nane usiku yeye yupo, siku zote yeye anavaa nguo ya fasheni ya kisasa zaidi na ndo mkufunzi wa sherehe zijitokezazo, maisha yake yalishazoea hivyo na furaha yake na maongezi yake yanategemea hafla kubwa ijayo. Mwanamke wa sampuli hii huwa huwezi kumfanya mwenza na kuhisi utajenga nae familia, labda wewe ndo uwe mtunzaji watoto na mchunga nyumba wakati yeye yupo bize usiku na masherehe.
6. Mpenda kupewa kipaumbele: Japo ni jambo la kike kutaka kupewa kipaumbele na jamii, ila ukiwa ni ugonjwa hapa lazima jasho liwe linakutoka kila siku, mwanaume mzuri ni yule anaemjali mkewe, ila kama mke yeye ndo anataka umjali yeye tu, kila ukitaka utoke anataka akuone, hujaenda kibanda cha kuangalia mpira jirani ameshapiga simu urudi anashida na wewe, yeye anataka ya kwake tu bila kuangalia hata wewe unahitaji muda wako binafsi wa mambo mengine, ukiwa na mwenza wa namna hii unakuwa mtuma kwake badala ya kufurahia nawe maisha yako jinsi unavyozeeka polepole, kuishi kwako inakuwa ili umtimizie shida zake yeye.
7. Mwanamke Mbea: Je Saa zote yeye hana ya kwake, anataka kujua flani anaishije na anafanya nini?, mwanamke wa namna hii haumuhitaji. Manaume huitaji mwanamke ambae anauwezo wa kujenga familia na hii inaitaji akili ambayo inauezo a kutatua matatizo yanayoizunguka familia yake, kama mwanamke akili yake ipo bize kuaza Mama Majuto nyumba ya pili leo wamekula nini haezi kua na akili ya kujenga zaidi ya kuongeza umasikini ka kutumia muda wake kusema na kuongelea juu ya wengine badala ya kufanya kazi za kimaendeleo, na utakuwa na wakati mgumu pia wa kumfanya akufikilie kuhusu wewe, unafika nyumbani yeye yuko mtaa wa pili kaendea umbea.
8. Mwanamke Mwenye Deko: Kuna wanawake wengine wameshazoea kudekezwa kwao, na hana tabia ya kufanya kazi ili aweze kujitimizia mahitaji maana hajakuzwa hivyo na hii siku zote haipo kwenye sifa ya mwanamke mzuri na mke mzuri, hata kama ukijitoa na kujitahidi kumpa maisha aliyokwisha zoea, jua kabisa ukimuoa watoto lazima watatokea kwenye familia, na mama mwenye deko hawezi kukuza watoto maana watoto wanahitaji kazi kubwa ya kuwaangalia na kuwakuza. Hivyo mwanamke wa namna hii hatoweza kuwa mwenza mzuri.
9. Mwanamke Ambaye Hana Msimamo: Mwanamke ambae huwa na hali ngumu kufanya maamuzi ya chochote, (kikazi, kijamii, kirafiki, kimahusiano au kwa vyovyote vile..) na hivyo hivyo hatokuwa na uwezo kwenye maamuzi hasa kwenye ndoa, maana atakuwa bendela kifata upepo, mtu akimwambia hiki yeye atakiamini, kile vile vile atafuata huko huko, na itakuwa ngumu pia kuwa mke mzuri maana dunia imejaa maneno mengi na vishawishi vingi.
10. Mwanamke Mwenye Mdomo Mchafu: Je ukigombana naye kidogo maneno yake yanakuwaje? maneno ya kebehi hayamuhishi, akikasirika hata heshima baina yenu inakuwa haipo tena?, vipi kuhusu watu wengine anaowaona wapo chini ya hadhi yake?, Kama majibu unayojijibu yanaelekea hana heshima kwa binadamu wenzake basi hapo umekanyaga bomu, litalipuka muda wowote na iwapo likilipuka lazima litakuumiza kihisia, na iwapo ukimfanya akawa mkeo basi kaka lazima kila jioni baada ya kazi utapitia baa ilio kalibu nawe. Na kiumeni.com inaendelea kukupa pole kwa kuyapa shida maisha yako ambayo yangekuwa matamu zaidi iwapo ungegunduwa mapema.
TAFAKARI KISHA CHUKUA HATUA!!

FUNZO LA MAISHA KWA VIJANA WA KIKE NA KIUME

Kijana mwenzangu usipite bila kusoma Love story (Stor yenye kugusa maisha)
Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.
Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!
Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.
Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini
Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!
Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!
Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.
Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu
Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.
Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!
Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.
----------------------------------------------------------------------
UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,
Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.
Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.
Kama unaamini Mungu anaweza kubadili maisha yako kwanini usiseme AMEN kisha
Share kwa wengine wajifunze

JIFUNZE KUMUACHA AENDE

Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.
MUACHE AENDE !
• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...
MWACHE AENDE !
• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...
MUACHE AENDE !
• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?
MUACHE AENDE !
• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...
MUACHE AENDE !
• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...
MUACHE AENDE !
• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...
MUACHE AENDE !
CHA KUJIFUNZA
• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!
• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.
NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Wednesday, 8 March 2017

HATUA 5 ZA KUZUNGUMZA NA MPENZI WAKO AKIWA AMEKASIRIKA


Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha.

Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya.  

Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana.

Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika.

MPUNGUZE MHEMKO
Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano.

Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi.

MSOME SAIKOLOJIA YAKE
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira.

Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira.

MRUHUSU AKUJIBU
Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake.

EPUKA MARUMBANO
Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena.

“Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano.

MUOMBE MSAMAHA
Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.”

Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako.

DALILI KUMI ZA KUKUJULISHA KUWA UMESHIKA MIMBA



Habari za leo mpenzi msomaji wa makala zetu, leo tunapenda kugusia kwa kiasi kidogo kuhusu dalili za mimba changa. Hili somo tumeamua kulileta baada ya wasomaji wetu wengi kuendelea kutuuliza maswali kuhusu namna mwanamke anavyoweza kugundua kuwa ni mjamzito hasa kwa akinadada ambao ndiyo mara yao ya kwanza kuwa katika hali hiyo.

Zifuatazo ni baadhi ya dalili ya mimba changa:
KWANZA. Mabadiliko katika siku zako(spotting). Unaweza kupata mimba na ukaendelea kuona damu mwezi huo. Hii hutokea yai lililorutubishwa linapojipandikiza katika kizazi. Mishipa ya damu iliyojaa katika ukuta huu tayari kulisha kiumbe huachia damu kidogo ambazo mwanamke anaweza kufikiri ni hedhi yake ya kawaida. Hata hivyo mabadiliko yataonekana kwani kiwango cha siku za damu hubadilika.

PILI. Kuongezeka ukubwa na kupata maumivu kwenye maziwa(chuchu). Hii inasababishwa na kuongezeka kwa homoni za estrogen pale unakuwa umeshika mimba. Hali hii huisha katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza.

TATU. Kichefuchefu na kutapika. Hali hii huwa mbaya zaidi wakati wa asubuhi unapotoka kulala. Na hii ni kwa sababu ya homoni za progesteron ambazo husababisha kupungua nguvu kwa msuli wa mrija wa chakula au koromeo.

NNE. Uchovu na usingizi usiokuwa wa kawaida na bila sababu. Hali hii husababishwa na ongezeko la homoni ya progesteron na mama utajikuta unapata usingizi kila mara. Hali hii huisha unapoanza mwezi wa nne wa mimba.

TANO. Kusumbuliwa na harufu mbalimbali. Hii hutokea hasa unapopata mimba ya kwanza utachukia harufu ya baadhi ya vyakula na vinywaji mbalimbali. Wakati mwingine hata harufu za baadhi ya watu zinaweza kukukera. Hapa kidogo panachekesha kwani baadhi ya akinamama huchukia hata harufu ya wapenzi au waume zao.

SITA. Kujaa gesi tumboni. Utaona baadhi ya nguo zako zinakubana zaidi sehemu ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya homoni nyingi mwilini zinakufanya kujisikia tumbo kujaa.

SABA. Kukojoa mara kwa mara. Hii hutokana na kuwa na damu nyingi mwilini ambayo huongezwa na homoni za ujauzito makusudi kutoa lishe ya kutosha kwa mama na kiumbe kilichomo tumboni. Kikemia ukiwa na damu nyingi mwilini utakojoa sana. Pili utajisikia kwenda sana haja ndogo mara nyingi pale kiumbe kitapoongezeka na kubana kibofu cha mkojo.

NANE. Kuongezeka kwa joto la mwili. Kwa akinamama ambao hupima joto lao kwa njia ya uzazi wa mpango, watagundua kuwa joto limepanda kwa muda wa wiki mbili au mbili na nusu mfululizo.

TISA. Kutoona siku zako za hedhi kabisa. Kwa akinamama ambao siku zao hazibadiliki au huenda vizuri yawezekana wakagundua pale wanapokosea siku na pengine kukimbilia hospitali. Hata hivyo kwa wale ambao siku zao hubadilika sana wataona ni kawaida ila kama ameshika mimba ataona mchanganyiko wa kichefuchefu, uchovu, kusinzia pamoja na kukojoa mara kwa mara.

KUMI. Kupima mkojo kwa kutumia kipimo cha karatasi ngumu. Pharmacy nyingi huuza vipimo ambavyo ukivichovya kwenye mkojo wako huweza kugundua homoni za mimba kwenye mkojo. Hii unaweza kupima mwenyewe ukiwa nyumbani au hata kazini. Kipimo hiki ukikichovya kwenye mkojo kama karatasi inavyoelekea utaona mistari baada ya dakika moja inajitokeza upande wa chini, ikitokea mistari miwili basi utakuwa una mimba na ukitokea mmoja itakuwa hauna mimba. Lakini kipimo hiki huwa kina changamoto zake kwa baadhi ya akinamama ambao kulingana na matatizo ya kiwango cha homoni mwilini hakitaweza kuonyesha majibu mpaka wapitishe wiki moja bila kuona siku zao.

Pamoja na dalili hizo hapo juu, ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu zaidi kutoka kwa daktari aliyepo karibu na wewe.

Monday, 6 March 2017

KWA WANAWAKE WOTE WANAOTARAJIA KUINGIA AU WALIOPO KWENYE NDOA




Ni jukumu lako kuwa romantic kwa mumeo. Aibu yako isikuzuie kuonyesha mapenzi yako kwa mume wako.
Mtumie meseji mume wako anapokuwa kazini, muda mwingine hata kama yupo nyumbani mnaangalia TV chati nae katika mitandao ya kijamii (watsapp, Imo, Facebook etc) hata kama yupo mbele yako.
Hii huleta faraja na ni njia mojawapo ya kuwa romantic kwa mwanaume wako. Jadiliana nae jinsi gani anavyokuvutia. Mnunulie zawadi hata leso, boxer, tai, viatu etc. Mnapokua mezani mkila pamoja labda nyama, mpe nyama kubwa kuliko zote.
Kama muda unao mtengenezee keki na juice ya matunda na msuprise nayo. Wadada, tumieni sauti yenu laini kumbembeleza na kumdekea, muimbie mnapokua pamoja chumbani, acheni userious kama mpo kwenye kikao cha bodi ya Korosho.
Mume wako anaporudi toka kazini usimkaribishe huku umenuna utafikiri shabiki wa Arsenal aliekosa kombe baada ya msimu wa ligi kuisha. Usimkaribishe mume wako huku mwili wako ukinukia mchuzi wa samaki au pilipili hoho, kuwa msafi na unukie. Wanaume hawapendi mwanamke mchafu.
Mkaribishe kwa kumkumbatia kila siku, na asubuhi anapoenda kazini Muombee Mungu amwepushe na mabalaa na muombee mafanikio. Msupport, mshauri, muondoe uchungu, mfariji pale panapokua na matatizo, sio kazi ndogo kuwa mwanaume.
Pale unapoona anapoteza matumaini ni kazi yako kumpa moyo ni wakati ambao anakuhitaji sana uwe karibu yake na sio kumkwaza tena. Usimfananishe na wanaume wengine. Mpikie chakula akipendacho, mfulie nguo zake, osha gari lake, mvalishe nguo na mpeti peti akiwa anaumwa.
Muamshe asubuhi na mapema, na usimlalamikie kama ana tabia ya kukoroma. Acha Kiss iwe njia yenu ya kuwasiliana. Mpe kitu inaitwa Morning glory (tendo la ndoa la asubuhi), hakikisha unamkamua vilivyo ili asitizame wanawake wengine pembeni! Soma vitabu kuelewa namna ya kuishi na mume, usijifunze kutoka katika movie. Ya kwenye Muvi Mengi sio ya kweli.
Muite mume wako jina lake la utani pia muite jina lake halisi hata kama ni mkubwa sana kuliko wewe as far as he is comfortable with it.
Msupport katika hobby zake, kama anapenda mpira jikite kuijua timu anayoishabikia, mnunulie jezi ya hiyo timu, kama mna watoto wananulie jezi ya timu anayoipenda baba yao na wavalishe. Usinune anavoenda kuangalia mpira. Mpira ni starehe kubwa sana kwa wanaume na huwafanya watengeneze marafiki kila siku!
Kumbuka Mwenyezi Mungu ameagiza wanawake kuwatii wanaume zao, hivyo basi mheshimu na kumtii hata kama ni mdogo kuliko wewe. Ndoa sio show off bali ni kujitoa kwa moyo wote. Hakuna jambo zuri kwa watu wawili wanaopendana kweli zaidi ya Ndoa na ukiona Mwanaume anasua sua kila ukimueleza suala la Ndoa, ujue huyo hayuko serious.
Na mwanaume ukipata mwanamke wa aina hii ni kwa nini uhangaike na michepuko iliyojaa laana ambayo ni mawakala wa shetani ktk kuvunja taasisi imara ya ndoa iliyoundwa na Mungu mwenyewe?
"To fall in love is a disease and its cure is to marry the person one is in love with. Love is when you take away the feeling, the passion and the romance and you find out you still care for that person."

NAMNA PEKEE YA KUEPUKA MAUMIVU KATIKA MAPENZI


Siku zote mapenzi yanapofika ukomo huwa na visa kibao hali inayopelekea maumivu yasiyokwepeka, hivyo basi kwa kuliona hilo Mtembezi Mahaba leo imekuandalia njia pekee za kukuepushia maumivu yasiyokuwa ya lazima katika mapenzi.
JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU: Hakuna jambo ambalo hutuliza fikra na hisia za mapenzi kama kukubali kumsamehe yule aliyekuudhi kabla hata hajakuomba msamaha na kuamua kusahau yote yaliyotokea. Yawezekana wengi mtasema haiwezekani.
Marafiki, lazima kila mmoja aelewe kwamba unapokasirika au kuumizwa, anayeteseka siyo yule aliyekusababishia maumivu bali ni wewe mwenyewe.
Hasira au maumivu ya kimapenzi huwa kama moto mkali ambao huitafuna taratibu nafsi ya mhusika. Ukisamehe maana yake unaupa moyo na akili yako nafasi ya kupata sehemu ya kutulia na kuuzima moto ambao tayari ulishaanza kukolea ndani yako.
BADILISHA MAZINGIRA/ MARAFIKI: Baada ya kuumizwa na mwandani wako, mbinu ya kubadilisha mazingira na marafiki husaidia sana kukupa nguvu ya kukabiliana na msongo unaoweza kukusababishia madhara makubwa.
Unaweza kubadilisha mazingira kwa kusafiri, kubadilisha mpangilio wa chumba chako cha kulala na kuondoa vitu vyote vinavyoweza kukukumbusha hisia chungu za maumivu. Taratibu utaona akili yako ikianza kusahau maumivu.
Yawezekana pia kuwa mpenzi wako ulishamtambulisha kwa marafiki zako nao wakamuona kama sehemu ya familia. Ukiendelea kujumuika na marafiki hao, watakuwa wanakukumbusha hisia chungu zitakazoendelea kukutesa, jiweke karibu na marafiki wapya wasiojua historia yako ya mapenzi, watakuwa sehemu ya faraja kwako.
JIPENDE, JITHAMINI: Utafiti wa kisaikolojia umebaini kuwa baada ya kutendwa kimapenzi, watu wengi hujishusha thamani na kudhani huenda wana upungufu, kasoro au udhaifu fulani ndiyo maana wapenzi wao wakawasaliti na kutoka kimapenzi na watu wengine. Kama ni mwanamke, muda wote atashinda kwenye kioo akijikagua kama ana kasoro kwenye sura na mwonekano wake. Mwanaume vivyo hivyo, atashinda akijiuliza kuhusu uwezo wake wa kumfurahisha mwenza wake faragha au uwezo wake wa kifedha.
Kujipenda na kujithamini kuende sambamba na kuboresha mwonekano wako, hakikisha muda wote unakuwa msafi na mazingira unayoishi pia yanakuwa masafi.
SITISHA MAWASILIANO: Unapokuwa na maumivu ndani ya moyo wako, jambo la busara ni kukaa mbali na kusitisha mawasiliano ya aina yoyote na yule aliyekusababishia maumivu hayo. Wengi hufikia hatua ya kubadili namba zao za simu ili kupata muda wa kutafakari mustakabali wa uhusiano wao.
Kama alikuwa rafiki yako kwenye Facebook au Twitter, ‘block’ mawasiliano naye, kama ni kwenye simu sitisha kumtumia ujumbe mfupi au kumpigiapigia simu, iache akili yako ndiyo iamue kama bado unahitaji kuendelea kuwa naye au la.
USITAFUTE WA KUZIBA PENGO: Kosa ambalo wengi hulifanya baada ya kutendwa na wapenzi wao, ni kukurupuka na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na watu wengine muda mfupi baada ya kuumizwa. Badala ya kupunguza maumivu, utajikuta ukiongeza ‘stress’ kichwani kwani huyo unayedhani atafaa kuziba pengo, anaweza kuwa na maovu kushinda hata huyo aliyekuumiza.
Jipe nafasi ya kukaa mwenyewe na kufikiria maisha yako ya baadaye, amini kwamba maisha yanawezekana hata ukiwa peke yako, kubaliana na kilichotokea na jiambie kuwa hutaki kurudia makosa kwa kuanzisha uhusiano na mtu atakayeuchezea moyo wako.
JIPE ZAWADI: Huenda wengi wakashangaa kwamba inawezekanaje kujipa zawadi mwenyewe? Inawezekana, tembelea duka linalouza zawadi za kimapenzi kama maua, kadi nzuri, midoli au chocolate na jichagulie unayoipenda zaidi. Jiambie kuwa hakuna anayekupenda zaidi ya jinsi unavyojipenda mwenyewe, jipongeze kwani maumivu hayatajirudia tena

KWA VIJANA WA KIUME MUNAOTAKA KUOA

Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo. Japo kila mtu anakasoro zake ila...