Saturday, 4 March 2017

MKE, FANYA HAYA KWA MUME WAKO




Muite kwa jina lake la utani...
Muache atumie mamlaka yake kama kichwa cha nyumba.
Usimcheke akiwa ameumizwa na jambo fulani.
Kaa kimya pale anapokuwa na hasira. Unaweza ukaenda kumuomba msamaha na kumueleza kwanini ulimkosea pale hasira zinapokua zimemuisha.
Kuwa na haraka ya kuomba msamaha pale unapokosea, sisitiza juu ya msamaha na mbusu pale anapokusamehe.
Ongelea mazuri yake na yeye kabla ndugu, jamaa na marafiki hawajafanya hivyo.
Waheshimu wazazi wake.
Msisitize kuhusu kwenda kuwasalimia wazazi wake na kuwapelekea chochote. Na afanye hivyo na kwa wazazi wako pia.
Msuprise kwa chakula akipendacho, hasa kipindi kile anapokuwa na msongo wa mawazo. Na kamwe usimcheleweshee chakula chake.
Usiruhusu dada wa kazi amhudumie chakula mume wako ukiwa nyumbani.
Mkaribishe kwa kumkumbatia anapotoka kwenye mihangaiko yake. Msaidie mizigo aliyokuja nayo au hata begi.
Tabasamu pale unapomtizama, vaa vizuri na jipendezeshe pale mnapotoka wote kwenda kwenye warsha mbalimbali.
Mpigie simu na kumchat asikuone Online akahuzunika
Kamwe usithubutu kutamka kuwa hakuridhishi kwenye  tendo la ndoa. Tafuta njia muafaka ya kufikisha ujumbe wako.
Mkumbatie tu bila sababu yoyote ile.
Mshukuru Mungu kwa kukupa Adamu wako katika maisha yako.
Kumbuka kumuombea na kumkabidhi mikononi mwa Mungu.
Tengenezeni utaratibu wa familia nzima kumshukuru Mungu kwa pamoja kila asubuhi na usiku kabla ya kulala
Mungu abariki ndoa zetu. Mlio single Mkapate wapenzi wenye mapenzi ya kweli leo na daima.
Na wasio serious na mahusiano wanaokupotezea muda wako wajikatae kwako mapema ili wasikuzibie nafasi ya kutimiza kusudi la Mungu kwako.
Kwanini tusiseme "Ameen "!
 Endelea kuwa na blog yako pendwa  kwa Makala mazuri ya kujenga na kuimarisha mahusiano na ndoa yako.

 Usisahau kucomment chochote ili tuendelee kuboresha.

No comments:

Post a Comment

KWA VIJANA WA KIUME MUNAOTAKA KUOA

Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo. Japo kila mtu anakasoro zake ila...