Saturday, 4 March 2017

MAMBO AMBAYO HUPASWI KUMFANYIA MWANAMKE ANAEKUPENDA KWA DHATI





1. Usimuumize moyo wake
2. Usi 'pretend' unampenda ili ufanikiwe kufanya yako.
3. Mtukane vyovyote... vile ila sio wazazi wake na kumwambia kuwa yeye ni mbaya.
4. Usimfananishe na wanawake zako waliopita.
5. Usimchukulie kirahisirahisi (Never take her love for granted)
6. Usimpige
7. Usimsaliti na kuonyesha kabisa dharau ajue kuwa una 'cheat'
8. Usimvunjie heshima kwa kumgombeza mbele za watu.
9. Usimpotezee muda wake kama hauna mpango wa kumuoa, unamchelewesha kupata mume bora.
10. Usimfanye ajione hapendwi na ana mkosi hapa ulimwenguni, huo ni ujuha.
11. Usimbake
12. Kamwe usisahau kumwambia unampenda na yeye ni mzuri hiyo haipunguzi nguvu za kiume.
13. Usimpe mimba na kumkimbia au kumwambia aitoe, kama huna nia ya kumuoa achana na hayo mambo, nadhani unajua kabisa matokeo ya kufanya ngono.

Sometimes sisi wanaume ni pasua kichwa vilevile, unakuta tunapata mwanamke anaekupenda kwa dhati, mwanamke ambae ni potential, mwanamke ambae hakodoi macho pochi yako, ila masikini ya Mungu anaishia kuumizwa na kulia kila siku na kujilaumu kwanini alikupenda.
Wewe fanya hivyo ukidhani unamkomoa, ila siku na wewe ukibananishwa na mwanamke mjasiriamwili utaisoma namba, nakwambia utauza hadi boxer.
Baadae unakuja kulalamika hapa 'wanawake wanapenda pesa, wanawake wanapenda pesa.' ukishikwa shikamana.
Na kama humpendi usimtongoze!

No comments:

Post a Comment

KWA VIJANA WA KIUME MUNAOTAKA KUOA

Hatari: Aina 10 za Wanawake Ambao Mwanaume Hafai Kuwa na Uhusiano Nao Zaidi ya Kujitakia Matatizo. Japo kila mtu anakasoro zake ila...